Skip to main content

A must read:-2025 Checklist

2025 checklist  1 1. Being kind and humble while not tolerating disrespect 2. Trying each time we fail or succeed 3.  More grass fed beef  4. More Avocados  5. More eggs 6. More early morning prayers 7. Early morning or evening in the Gym 8. More Kefir  9. More books 10. No seed oils  11. No sugar 12. No wheat 13. No alcohol 14. More cruciferous vegetables  15. More intermittent fasting  16. More sauerkraut  17.  No TV 18.  Proper hydration with a pinch of pink Himalayan salt  19. More walking with a target of 10000 steps daily. 20. No BJs . No CJs. Your mouth is not a sexual organ. Mahali gynaecologist anatumia mask , gloves Na speculum wewe unataka kutumia mdomo na ulimi yako kama litmus paper  21. No processed food 22. No small goals  23. Block ijiots  24. More peace. More happiness 25. More friends with benefits  2025 Checklist 2 1. Quit all dowry/ rûracio WhatsApp groups. Respect your wife by working fo...

Dedication to our defence forces

Tunalala kwenye vumbi na matope ili wewe ulale kitandani,
Tunala na bunduki ili wewe ulale na mwenzi wako,
Tunalala porini ili wewe ulale kwenye nyumba,
Unavaa kofia maridadi ya kupendeza, sisi tunavaa kofia ngumu na nzito za chuma,
Unavaa "vest" nzuri ya pamba, sisi tunavaa "vest" za shaba,
Unavaa mkanda wa ngozi kiunoni, sisi tunavaa mikanda ya risasi,
Asubuhi unaamshwa na "alarm" nzuri ya simu yako, sisi tunaamshwa na milio ya mabomu na risasi,
Unatembelea gari zuri la thamani, sisi tunatembelea vifaru na malori,
Unakula chakula kizuri ukipendacho, tunakula wadudu na matunda porini,
Tunakesha ili wewe upate usingizi,
Tunaua ili wewe uishi,
Tunaumia ili wewe upone,
Tunaitoa sadaka "leo yetu" kwa manufaa ya "kesho yako",
Tunatoa sadaka maisha yetu ili kutetea maisha yako,
Tunakupigania usiku na mchana kwa sababu tunakupenda,
Tunaipenda nchi yetu,
Sisi ni wanajeshi,
Sisi ni wazalendo,
Sisi ni mashujaa,
Ombea wote waliofia vitani,
Wamekufa wakitetea nchi yetu,
Wamekufa wakitetea uhai wako,
Ni mashujaa wetu,
Nchi yetu,
Amani yetu,
Jeshi letu.
DEDICATE TO OUR DEFENCE FORCE....
"FOR GOD AND MY COUNTRY" One of the words of the frontline KDF

Comments