Skip to main content

KTN's investigative journalist Mohamed Ali open letter to the president about the security issue in kenya

KTN's investigative journalist Mohamed Ali wrote the president a letter in Swahili about the security issue in the country.Read the letter below: Rais,Habari ya siku nyingi? Jina langu ni Mohammed Ali, mwandishi wa habari ya runinga ya KTN. Mara ya mwisho kuonana naye ilikua wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita huko Mombasa katika shule ya msingi ya Khadija. Ulikua mchangamfu kando na ahadi chungunzima kwa Wakenya. Ahadi za tarakilishi za bure kwa wanafunzi wa darasa la kwanza, kutoa nafasi za kazi milioni moja kila mwaka kwa vijana, kuekeza katika usalama wa kitaifa miongoni mwa ahadi zingine. Lakini, kwa hivi sasa bwana rais nahofia ahadi hizo zimekua tasa. Barua yangu inaanza na maswala ya usalama ambayo nimeyapa kipau mbele. Kwanza kabisa nauliza, “Uko wapi? Hatukuoni bwana Rais.” Wakenya wanashabuliwa kila mara na kuuliwa kinyama. Walioponea wamebagi na vilema vya maisha. Shambulizi la Westgate na ahadi ya serikali yako zilionekana kama hekaya za Abunuasi. Uliowapa majukumu ya kutulinda wako wapi? Kuanzia Mkurugenzi wa NIS, Michael Gichangi, Inspekta Jenerali wa Polisi, David Kimaiyo, Mkurugenzi wa CID, Ndegwa Muhoro, Kamanda wa GSU, Kitili Mboya, Waziri wa Usalama wa Ndani, Joseph Ole Lenku na Mkuu wa Majeshi, Julius Waweru Karangi. Ukweli wa mambo ni kwamba Wakenya wanahisi kuwa nyote mmelala. Usalama umegeuzwa na kuwa mchezo wa tufe. Tumejisahau kiasi cha hata kuonyesha siri zetu za ndani kwa maadui zetu. Hatujui tunapigana na nani. Katika kazi yangu ya uandishi wa habari, nimezungumza na wadadisi wa maswala ya usalama na bwana Rais wengi wao wanahisi twapigana wenyewe kwa wenyewe. Na iwapo si wenyewe kwa wenyewe basi twafukuzana na kivuli cha fimbo ambacho hakisitiri jua. Badala ya kuua magaidi tunajiua wenyewe kwa wenyewe. Kwa kweli hatuwezi shinda vita hivi ikiwa twaumizana wenyewe kwa wenyewe badala ya kuungana. Mara tunaambiwa ni MRC, mara ni Mungiki, mara magaidi, maragodoro na sasa waziri wako Ole Lenku ana mapya zaidi. Waswahili wanasema “Bata ata umlishe mawe bado atahara”. Bwana Rais, tumwamini nani? Bwana Rais, majuzi uliingia na taswira mpya kabisa katika uwanja wa Nyayo; magari ya kujikinga na risasi na usalama zaidi. Hii, si kawaida tangu uongozi wa Hayati Mzee Jomo Kenyatta, Daniel Toroitich arap Moi na Mwai Kibaki. Iwapo wewe unahofia, je sisi walalahoi tutahisi vipi? Mauaji ya Mpeketoni ni sawia nay ale ya Tana River. Damu ya wana Mpeketoni inalilia haki. Kina mama wamechwa bila watoto na waume huku watoto wakisalia mayatima kwa kosa la serikali walilolichagua ki katiba, serikali iliyowaahidi kuwalinda pamoja na mali zao. Mauaji ya kiholela yanazidi kugonga vichwa vya habari, baadhi ya walinda usalama wameamua wao ndio majaji na mawakili kwa Wakenya wanyonge wasio na mtetezi. Bwana Rais, wakenya wanalia; kuanzia Easatleigh, Baragoi hadi Mandera. Nina machungu na mengi ya kukueleza lakini muda hauniruhusu. Kumbuka Kenya ni jina, nchi ni sisi. Ni hayo tu kwa sasa. Shukran

Comments

Popular posts from this blog

MOURNING THE ONLY PRINCIPAL I KNEW

By Dr.Paul Bundi Karau I arrived at Kanyakine High School on 18th February 1999 a small village boy. I had never been to a boarding school, and certainly this is the furthest from home I had ever gone. The boys who were assigned to escort me to Mungania dorm looked at my stunted height and loudly wondered how I would survive in Beast's school.  "Who is Beast?" I asked in bewilderment. "You will know." Musyoki answered curtly. It didn't take me long to know who Beast was. The following day, as the 10 o'clock tea was being served, I heard a commotion, with boys leaving their tea and running helter-skelter towards the classrooms.  I was a fresh mono, so I didn't know what was happening. I ran along the pavement, and came upon a mighty man, who appeared to be adjusting his trousers. He yanked his belt and thrust one whip towards me. I had encountered Beast himself. He was tall, imposing, burly and endowed with a thunderous voice that could re...

Political Tumbocrats

*Political Tumbocrats* A political tumbocrat is a person who hangs around elected leaders to satisfy her/his personal greed. Tumbocrats sees a leader as a demigod whom they worship. The r bootlickers and sycophants of the highest order. Their work is to defend leaders and cheat public that something is happening. A tumbocrat has no values or morals. A tumbocrat is not interested with common good but personal good. A tumbocrat has no vision but appetite for being near high table of power  and feeding on crumbs.   Tumbocrats are greatest obstacles to development in our country. They protect the corrupt and shield the bad governance in so far as they get something to fill their tumbos. They are good and articulate in arguments but they lack the moral authority because they don't value truth. Every political leader is surrounded by tumbocrats. They are the noise makers in social media and around leaders defending them. They peddle lies en create propagandas . They confuse the publ...